SAMATA ANENA JUU YA DOMAYO NA SURE BOY.
SALUM Abubakari na Frank Domayo ni wachezaji ambao wameleta mapinduzi makubwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Hiyo ni kutokana na vijana hao kucheza kwa kiwango kikubwa kwenye safu ya kiungo.
Mshambuliaji, Samatta amekiri kuwa vijana hao licha ya kuwa na maumbile madogo wanafanya kazi yao ipasavyo.
"Jamaa wapo vizuri. Ukiwatazama maumbile
yao na kazi ambayo wanaifanya ni vitu viwili tofauti." alisema Samatta
anayekipiga na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Katika mchezo wa Stars na Morocco
uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi Jumapili kusaka
kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Brazil mwakani.Stars ilishinda mabao
3-1.
Kiungo Salum Abubakari wa Azam FC
aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo mchezeshaji alipiga jumla ya pasi 66
wakati Frank Domayo wa Yanga aliyecheza nafasi ya kiungo mkabaji
alipiga 54.
Kati ya pasi 66 alizopiga Sure boy kwenye mchezo huo. Pasi 56 zilikuwa sahihi wakati 10 zikipotea njia.
Frank Domayo aliyekuwa na jukumu kucheza
nafasi ya kiungo mkabaji, alipiga jumla ya pasi 54. Kati ya pasi hizo
48 zilikuwa sahihi wakati sita zilienda fyongo.
Pia, Domayo alipiga mashuti matatu kwenye lango la Morocco huku Sure boy akijibu kwa kufumua mashuti mawili.(Habari na hisani ya www.shaffih.blogspot.com )
No comments:
Post a Comment