BITTEVIEW;JINA LAKO HALISI WAITWA NANI?
HUMUD;NAITWA ABDULHARIM HUMUD GAUCHO
BITTEVIEW;UMEZALIWA LINI NA WAPI?
HUMUD;NIMEZALIWA ZANZIBAR MWAKA 1987
BITTEVIEW;NI LINI ULIANZA KUIKAMILISHA SAFARI YAKO YA KUCHEZA SOKA?
HUMUD;MPIRA NIMEANZA KUCHEZA SIKU NYINGI TANGU NIKIWA MDOGO HASA SHULE NILOSOMA ZANZIBAR KIEMBESAMAKI.
BITTEVIEW;UNA NDUGU YAKO ALIYEFUATA NDOTO KAMA ZAKO?NA KAMA YUPO YU WAPI KWA SASA?
HUMUD;NAO NDUGU ZANGU WAWILI AMBAO NAO WANACHEZA MPIRA MKUBWA AKIITWA FEISAL ALIWAHI KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA OMAN NA MWINGINE YUPO KLABU YA HUKO OMAN INAITWA SIB CLUB
BITTEVIEW;UMEOA?NA UNA WATOTO WANGAPI?
HUMUD;NIMEOA NA NA MTOTO MMOJA ANAYEITWA MUNIR
PICHANI NDO MUNIR MTOTO WA KIUNGO HUYO ANAYEKIPIGA AZAM.
BITTEVIEW;UNAIONGELEAJE KLABU YAKO YA AZAM?
HUMUD;NI MOJA YA KLABU AMBAYO ALISTAHILI KILA MCHEZAJI KUCHEZA KWANI NI MOJA YA KLABU BORA KABISA UKANDA HUU IKIJALI KILA KITU AMBACHO MCHEZAJI ANATAKIWA KUPATA.
BITTEVIEW;NI MCHEZAJI WA AZAM AU LIGI KUU NZIMA UNAYEMKUBALI KULIKO WOTE?
HUMUD;KUSEMA UKWELI NAMKUBALI SANA KHAMIS NCHA VIALLI
BITTEVIEW;LABDA NI NDOTO YA KILA MCHEZAJI KUCHEZA ULAYA KWAKO HILI LIMEKAA VIPI?
HUMUD;SIKU ZOTE NDOTO YANGU IMEKUWA KUCHEZA ULAYA SO BADO SIJAKATA TAMAA NA NAAMINI KWA UWEZO WA MWENYEZIMUNGU NTAFANIKIWA.
BITTEVIEW;KIPINDI CHA MAXIMO ULIWAHI KUGEUKA LULU KWA MBRAZIL YULE LAKINI KUJA KWA KIM POULSEN KUMELETA KUENGULIWA KWAKO?
HUMUD;NAHISI NI KUTOKANA NA MIMI KUTOCHEZA HATA KWENYE TIMU YANGU YA KLABU JAPO NATARAJIA KUFANYA MAJARIBO JOMO COSMOS YA SAUZI
BITTEVIEW;ZAMANI TULIKUZOEA KWA MITINDO YAKO TOFAUTI YA KUSUKA JAPO SIKU HIZI IMEKUA TOFAUTT ,NI KWELI MKEO ALIKUZINGUA KUHUSU WEWE KUSUKA?
HUMUD;NI KWELI AMEKUWA HAPENDI MI NISUKE NA NDO SABABU SIKU HIZI NANYOA NA HII NI KWA MAPENZI YANGU KWAKE
BITTEVIEW;WE NI MMOJA KATI YA MATUNDA YA SHULE YA SEKONDARI MAKONGO?JE NI WANAFUNZI GANI ULOSOMA NAO NA WAKO WANAKIPIGA BADO?
HUMUD;NAWAKUMBUKA HENRY JOSEPH SHINDIKA,JUMA JABU,JUMA ABDUL NA JERRY TEGETE.
BITTEVIEW;NIMEKUZOEA MARA NYINGI KAMA KIUNGO WA KATI,NI NAMBA ZIPI UNAZOWEZA KUZICHEZA UKIACHA KATIKATI?
HUMUD;NA UWEZO WA KUCHEZA NAMBA 4,5,10 NA 11
BITTEVIEW;KWA NINI WANAKUITA "GAUCHO"?
HUMUD;JINA HILO NILIPEWA NA WASHABIKI WA ASHANTI PENGINE NI KUFANANA KWANGU NA GAUCHO JAPO PIA NAMPENDA SANA MCHEZAJI HUYO NA NI ROLE MODEL WANGU
HUMUD;NI BARCELONA YA HISPANIA NA LIONEL MESSI NDO KIPENZI CHANGU.
BITTEVIEW;NI MECHI GANI AMBAYO HUWEZI ISAHAU KATIKA MAISHA YAKO YA SOKA MPAKA SASA?
HUMUD;NAFIKILI NI ILE YA BRAZIL NA IVORY COAST SANASANA NIKIWA NA TIMU YA TAIFA.
BITTEVIEW;ULIONEKANA KUPANIC NA KUJAA JAZBA BAADA YA GAME NA IVORY COAST JAPO ULIKUWA NYOTA WA MCHEZO HUO?
HUMUD;HALI ILE ILILETWA BAADA YA MCHEZAJI WA IVORY COAST ARUNA DINDANE KUNILETEA UKOROFI KIPINDI CHA DAKIKA 90 NDO NA MI NIKAMPANDISHIA SI UNAJUA TENA HASIRA ZA KIARABU.
BITTEVIEW;PENGINE NI MTU AU WATU GANI AMBAO LAZIMA UTAWASHUKURU MPAKA HAPA ULIPOFIKA UKIACHA FAMILIA YAKO?
HUMUD;NAHISI NI KANALI IDDY KIPINGU ALINIFANYA NIUPENDE SANA MCHEZO HASA KIPINDI KILE NASOMA MAKONGO DAR
BITTEVIEW;UNAPENDA SANA MUZIKI WA HIPHOP,JE NI MWANAMUZIKI GANI AMBAYE UNAMKUBALI SANA HAPA BONGO?
HUMUD;NAMPENDA SANA FAREED KUBANDA A.K.A FID Q
BITTEVIEW;EBWANA TUNASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WAKO NA MUNGU AKUJALIE,KILA LA KHERI.
HUMUD;KHERI SANA NA PAMOJA SANA KAKA.
No comments:
Post a Comment