Tuesday, March 26, 2013

SAMATA MATUKIO KUMI YA PICHA

           MBWANA ALLY SAMATA

                                                


Samata wanne kutoka kushoto kati ya wale walosimama hapo akiwa na kikosi cha KIMBAGULILE F.C ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
                        
Akiwa ndani ya uzi wa Msimbazi,Simba Sports Club baada ya kusaini kuichezea klabu hiyo akitokea African Lyon ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Mohamed Dewji kipindi hicho.
                               




Picha mbili zikionyesha kuwasili kwa Samata nchini Congo na kutambulishwa kwake rasmi klabuni hapo na mmiliki wa klabu hiyo bwana Moisseh Katumbi. 
                       
Mungu akajalia na kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira wa Tanzania akawa mtanzania wa kwanza kuichezea klabu ya TP MAZEMBE ya Congo na kisha kuweka historia mbalimbali katika tasnia yake ya soka ambapo ameweza kucheza pamoja na wachezaji wenye historia kubwa Afrika kama Tresor Mputu,Kidiaba,Deo Kanda,Given Singuluma,Reinford Kalaba,Stopilla Sunzu na wengine wengi.
  Samata ameweza kutengeneza jina kubwa jijini Lubumbashi na klabu yake ya TP MAZEMBE ambapo mwaka jana aliweka rekodi kuwa mmoja kati ya wafungaji bora wa klabu bingwa Afrika akiwa na magoli sita na kuwa mfungaji bora wa klabu ya klabu yake.
                     
Alimkosha sana Didier Drogba baada ya mechi hii ilopigwa Ivory Coast ,hongera kaka umekuwa balozi wa kweli wa mpira Tanzania.
                   
  Kwao Mbagala alikokuimba Diamond kuwa kuna majalala ila siku hii Asou Ekoto alikuwa na kazi ya ziada.
             
 Aliwatesa sana waarabu wa Al ahly yaMisri na Esperance ya Sudan kikubwa anatembea na Utanzania moyoni mwake.
                                 


               
 
                                 
                
                                                                                             

                                                           
Nia ya picha hizi ni kuonyesha jinsi alivyowatesa mabeki wanaokipiga ligi mbalimbali za Ulaya,hii ikiwa changamoto kwa wachezaji wote kwamba tukijaribu kumbe tunaweza.
                 Kipindi mdogo nilikuwa nikishangaa kwa nini washabiki walikuwa wakimuona David Beckham lazima wamkimbilie awasainie chochote kile iwe jezi,kitabu au hata mwili nahisi ni umaarufu wake na leo ndo hichi nachokiona hapa,hii ilikuwa Ivory Coast washabiki walimkimbilia Samata.
                  
Matunda ya miguu yake miwili,nguvu kidogo na akili zake nyingi pamoja na dua za wenye kumtakia heri.
                   KILA LA HERI KAKA
                    

              

                            

No comments:

Post a Comment