Jana usiku Chelsea waliibuka lulu ndani ya dimba la ELLAND ROAD uwanja wa nyumbani wa Leeds United katika mchezo wa robo fainali ya CAPITAL ONE.

Chelsea walitoka nyuma baada ya kufungwa goli moja dakika ya 37 na mshambuliaji wa Leeds Ashdown na ikawabidi kusubili hadi dakika ya 53 ambapo Mapa aliisawazishia Chelsea kwa mpira hafifu baada ya kupata pasi toka kwa Moses na Chelsea wakawa kama wameamka tena tangu walipotoka mapumziko baada ya kupokea neno toka kwa kocha wao Rafael Benitez,

Ashdown goal
Mata's goal with azpilcueta
Chelsea waliongeza nguvu baada ya kumuingiza Kiungo wao mshambuliaji mbelgiji Eden Hazard aliyebadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa na kona iliyopatikana dakika ya 64 ikapigwa na Lampard ilizaa bao lililofungwa na beki wa kulia wa Chelsea Ivanovich na dakika tatu baadaye Kazi nzuri ya mnijeria Moses ilizaa bao la tatu baada ya kuachia kombora kali dakika ya 67 hivyo ubao wa matokeo kusomeka Chelsea 3 Leeds 1
Ivanovich with the 64' goal
Again Moses
Chelsea waliwasakama Leeds mpaka baadaye El ninho Ferdnando Torre aliposhindilia msumali wa nne na Mata akahitimsha bao tano hivyo Chelsea kufuzu kwa hatua ya Nusu fainali ya C apital one

Hazard scoring.
NILFURAHI KUMUONA DIOUF japo zama zake zimeenda saana kwani Diouf niliyemuona jana ni wa tofauti sana na yule niliyemwona mwaka 2002 Korea na Japan kombe la dunia akiwa na uzi wa Senegal japo ni mmoja wa watu naowakubali saanaa.
No comments:
Post a Comment