Thursday, March 28, 2013

SASA ABDULHARIM GAUCHO KUKIPIGA JOMO COSMOS

          HUMUD KUKIPIGA SAUZI
                                           
Kiungo mwenye mapafu ya mbwa Abdulhalim Humud Gaucho huenda akasafiri kuelekea bondeni Afrika ya Kusini wikiendi hii kufuatia kupata nafasi ya majaribio kwenye timu ya Jomo Cosmos aliyowahi kuchezea watanzania mengine Nteze John na Ally Shah siku za nyuma
Cosmos inayomilikiwa na kocha wa zamani wa Bafana Bafana Jomo Sono imempa nafasi hiyo humudi baada ya kufanyiwa mipango na uongozi wa Azam FCkatika kutekeleza sera yake ya kutengeneza uwanja mkubwa kwa wachezaji wa kitanzania kwenye ligi mbalimbali zinazoendeshwa kisasa.
Cosmos ambao wapo kwenye kampeni ya kurejea PSL watahitaji huduma ya Humud msimu ujao ambao Jomo Sono ameahidi kuwa watakuwa wakicheza PSL.Humud ataungana na wachezaji kama Mbwana Samata,Ulimwengu,Henry Joseph wanaocheza mpira wa kulipwa nje.
Humud aliyewahi kuzichezea Ashanti,Mtibwa Sugar ya Morogoro kabla ya kutimkia msimbazi Simba Sports Club na baadaye Azam FC atakumbukwa zaidi kwa makubwa aloyafanya siku ya mechi ya Tanzania na Ivory Coast jijini Dar ambapo siku hiyo alipiga mpira mwingi mpaka Dindane Aruna kutoka mchezoni na kutaka kugombana.KILA LA KHERI KAKA 

No comments:

Post a Comment