Timu ya taifa ya Tanzania leo itarusha tiketi yake ya kugombania kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwakani 2014,Ikumbukwe kwamba Tanzania wanaingia uwanjani wakiwa na saikolojia nzuri kufuatia matokeo mazuri waloyapata baada ya mechi za kirafiki walizocheza na Zambia na kushinda bao moja lilowekwa kimiani na Mrisho Ngasa na ile dhidi ya Cameroon lilofungwa na Mbwana Ally Samatta"POPA" naileta hii hoja ya SAIKOLOJIA kuwa pengine inaeza ikawa chachu na sababu ya kuibua morali kwa wachezaji wa Tanzania na hadi kupata matokeo tukichukulia kwamba timu kama Zambia na Cameroon ni moja ya timu bepari kwenye mpira wa Afrika ukikumbuka kwamba Zambia walikuwa mabingwa mwaka 2012 wa mataifa Afrika.
Labda utofauti wa hizi mechi za kirafiki na hii ya leo dhidi ya Moroco ni kwamba mechi ya leo ni ya kimashindano zaidi na kila timu ikitafuta pointi tatu muhimu ambapo Tanzania wakishikilia nafasi ya pili na Moroco ya tatu katika msimamo wa kundi hilo.
Mechi ya kwanza,Tanzania walipigwa bao mbili na Ivory Coast jijini Abdijan kabla kuwafunga bao mbili Gambia jijini Dar es Salaam hivyo kujikita katika nafasi ya pili na pointi zake tatu.
FALSAFA YA KIM POULSEN;
Kocha huyu mwenye kupenda kutumia mchezo wa pasi fupi na nyingi maarufu kama samba ukichezwa na timu kama Brazil na Hispania ambapo mara nyingi amekuwa akitumia viungo wake MWINYI KAZIMOTO,FRANK DOMAYO,ABUBAKAR SALUMU"sure boi" Ambayo kiukweli wamekuwa chachu kwa timu pinzani mara zote wanaposhuka uwanjani huku mashindano ya chalenji nchini ya Uganda mwaka jana yakiwa kithibitisho hai,JE LEO HII WATAWANYANYUA WATANZANIA?
UWEPO WA SAMATA NA NGASSA
Silaha hizi mbili ndo zilizokuwa sababu ya Zambia na Cameroon kurudi vichwa chini,uwepo wao kwenye kikosi unaibua mashambulizi na matumaini kwa timu hiyo kwani ni watu wenye uwezo wa kubadili matokeo saa yoyote...
KAMATI YA ULINZI CHINI YA YONDANI,NYONI,KAPOMBE,AGGREY MORRIS NA MAFTAH;
Mara ya mwisho tunacheza na Gambia,NYONI na KAPOMBE ndo walofunga magoli mawili ya Stars huku wakifungana vyema nyuma kuhakikisha ulinzi unakuwepo chini ya mkandarasi mkuu nemanja Vidic,KELVIN YONDANI na beki mzoefu AGGREY MORRIS.
CAPTAIN J.K.JUMA
Akiongea na waandishi wa habari jijini dar alinadi,"Timu imejiandaa vizuri na wako katika hali nzuri ya mchezo pia akasema wanaiheshimu Moroco na wanatambua ni moja ya timu kubwa barani Ulaya lakini mwisho wa siku ni wachezaji kumi na moja tu ndo wanaoingia uwanjani basi hivyo watapambana hadi mwisho wa mechi"
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI TAIFA STARS.
No comments:
Post a Comment