Thursday, December 20, 2012

HOTELI KUBWA YA KITALII YAFUNGIWA DAR;NI AGIZO LA WAZIRI DR,THEREZYA

                         WAZIRI DR.TEREZYA AONYESHA MAKUCHA YAKE.                
                                                       

 


WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, ameifunga Hoteli ya Kimataifa ya Double Tree, ya jijini Dar es Salaam, kutokana na kitendo cha kutiririsha maji machafu baharini.

Dk Huvisa alifanya hivyo jana baada ya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu wake, Charles Kitwanga.
Waziri alitembelea hoteli hiyo ili kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara katika viwanda na hoteli zilizoko pembezoni mwa bahari, ili kuona mfumo wa majitaka.

Nawataka kurekebisha mara moja mfumo huo wa majina kulipa faini kwa Baraza la Hifadhi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc),”alisema Dk Huvisa.

Dk Huvisa alifika hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa agizo lililotolewa na naibu wake wiki mbili zilizopita, halijafanyiwa kazi.

Alisema hoteli hiyo itafungwa hadi hapo itakapotekeleza agizo hilo na kuhakikisha kuwa majitaka hayatiririki baharini kama ilivyo sasa.
                          



Doubletree By Hilton Dar Es Salaam - Oysterbay Hotel And Outdoor Pool
                                             Hii ilifuata katika ile ya hali ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa vyema mfano hai ni chanzo cha kikubwa cha maji kama bahari na ni aibu kubwa kwa hoteli kubwa kama hii kuwa chanzo hai cha kukarbisha uchafu kwenye vyanzo hai vya maji kama hivi.Sisiti kumpongeza Dr.Therezya kwa hatua ya kishujaa alochukua. hapa kwa kweli NEMC wamenena
                                           



 
 

No comments:

Post a Comment