Wednesday, December 19, 2012
ZIZZOU ANATISHA; RONALDO'S FRIENDS YAIKANDAMIZA ZIZZOU'S FRIENDS BAO TATU MECHI YA HISANI
ZINEDINE ZIDANE ANATISHA
Katika hali ya kushangaza kabisa mchezaji bora mara mbili wa dunia na raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria Zinedine Zidane maarufu kama Zizzou jana aliwastaabisha watu walioudhuria mechi ya hisani maalumu ya kupinga umaskini iliyochezwa nchini Brazil ambapo viliundwa vikosi viwili yaani RONALDO'S FRIENDS chini ya gwiji Ronaldo De Lima na ZIDANE'S FRIENDS chini ya Zidane mwenyewe aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu licha ya kwamba alistaafu mwaka 2006 na historia ya kumpiga kichwa beki wa Italia Matterrazi na Ufaransa kupoteza fainali hizo mbele ya waitaliano.Mechi hiyo iliishia kwa RONALDO'S FRIENDS kuibuka na ushindi wa mabao matatu(3) yalowekwa kimiani na BEBETO,FUSTAR na CAFU kwa mawili(2) ya ZIDANE'S FRIENDS yaliotupiwa na Zidane pamoja na Falcao.(magoli haya hapa)
http://www.youtube.com/watch?v=A6ckI0HbVLk&feature=player_embedded#t=0s
Mechi ilijumuisha mastaa kibao wanaosakata kabumbu sasa na zamani hivyo kubeba mvuto wa aina yake jana hiyo.
RONALDO'S FRIENDS;DANRLEI,DIDA,CAFU,SERGINHO,JUNINHO,ROBERTO CARLOS,WILLIAM,LUCAS,PAULISTA,ZINHO,DENILSON,RONALDO,NEYMAH,LEONARDO,
CACA,BEBETO,ROMARIO,EDMUNDO.
ZIDANE'S FRIENDS;VICTOR,JULLIANO,BELLETTI,DIEGO CAVALIERI,EMERSON,FERNANDO HIERO,SALGADO,JUAN PABLO SORIN,MONTERO,HIDETOSHI NAKATA,ZIZZOU,DECO,SANTIAGO SOLARI,ROMAN RIQUELME,CHRISTIAN KAREMBEU,ALEX DE SOUZA,PEDRO PAULETA,SEBASTIAN ABREU,HULK,FALCAO,MARIO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment