MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA ST.ANTHONY 2012-2013

Mgeni rasmi katika mahafali ya
20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa shule hiyo
kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hizo.
Padri akiendesha ibada wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa akifuatilia ibada hiyo kubariki mahafali ya 20 ya kidato cha sita
ya Shule ya Sekondari St. Anthony. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo
Sylvester John na Mkuu wa shule hiyo Bro. Ismail Edward ( wa pili
kulia).
Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya St. Anthony wakisikiliza mahaburi wakati wa ibada hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kwenye sala maalum wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakisoma sala za mtu mmoja kuombea mambo tofauti ikiwemo Amani kwa Taifa.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha
Sita shule ya Sekondari St. Anthony wakimwogoza mgeni rasmi kwa madoido
ya aina yake wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa akiwasili katika viwanja vya shule ya Sekondari St. Anthony akiwa
ameambatana na viongozi wa shule hiyo tayari kuanza rasmi sherehe za
mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakishiriki kuimba wimbo wa shule.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato
cha tano wakiimba wimbo wa kuwaaga dada zao na kaka zao mbele ya mgeni
rasmi wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari St. Anthony wakifanya igizo la Dr. Livingstone lililowavunja mbavu wazazi na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa akiwa hoi kwa kucheka kutokana na igizo la Dr. Livingstone.
Kushoto ni Makamu Mkuu wa pili wa Shule hiyo Rempta Adams akifuatiwa na
Mkuu wa Shule hiyo Bro. Ismail Edward.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya
sekondari St. Anthony Rempta Adams akisoma taarifa ya shule hiyo mbele
ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo amezungumzia
changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na uhaba
wa vifaa vya kufundishia na kujifunza, mabadiliko ya mara kwa mara ya
Mitaala na matamko juu ya Elimu, tabia ya wanafunzi kuiga tamaduni za
Ughaibuni na Ukosefu/kukatika kwa nishati ya Umeme.
Sehemu ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akikabidhi taarifa ya shule yake kwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa
St. Anthony Jacqueline Ndunguru akisoma risala ya wanafunzi wa kidato
cha sita mbele ya mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akimkabidhi mgeni rasmi risala hiyo.
Mwanfunzi Samwel Mwanzini akionyesha kipaji chake cha kuimba na kupiga kinanda ambapo alishangaza wengi kwa uwezo aliokuwa nao.
Mwanfunzi Tracy Raymond
Ndanshau wa kidato cha tano PCM akiimba sambamba na Mwl. Nikiza Bwenge
katika mahafali ya 20 ya kidato cha sita.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo
Sylvester John (kulia) akisoma risala fupi ya kukabidhi wahitimu kidato
cha sita 2013 kwa wazazi rasmi Bw. na Bibi Amos Bujiku wakati wa
mahafali hayo.
Wazazi rasmi rasmi Bw. na Bibi
Bujiku wakiwapokea rasmi wanafunzi Mary Bujiku na Edward Mugyabuso kwa
niaba ya wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuwalea kiroho.
Mkuu wa Shule ya sekondari St.
Anthony Bro. Ismail Edward akisoma risala kwenye mahafali ya 20 ya
kidato cha sita ambapo amewasihi wanafunzi wanaohitimu waendelee kutunza
kumbukumbu ya shule hiyo na kuwa mabalozi wazuri wa St. Anthony kwa
kuwa wazalendo wa kweli waliotayari kulijenga na kulilinda taifa letu na
kukabiliana na changamoto za dunia ya leo hususani gonjwa hatari la
Ukimwi na matatizo mengine yanayoikumba Tanzania.
Meza kuu ipitia risala ya Mkuu wa shule hiyo.
Picha juu na chini Mgeni rasmi
Mstahi Meya Jerry Silaa akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya kidato
cha sita ya St. Anthony ambapo ametoa pongezi kwa walimu na wanafunzi wa
shule hiyo na kuongeza kuwa kwa sisi Watanzania Elimu ni nyenzo muhimu
sana hasa katika mbio zetu za kupambana na maadui watatu; ujinga,
maradhi na umaskini ambayo ni Silaha pekee ya kuwashinda maadui hao wote
watatu.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Wahitimu wa kidato cha sita wakielekea kukabidhi zawadi kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea zawadi hiyo.
Mgeni rasmi akifingua zawadi hiyo mbele ya wahitimu hao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa
akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na wahitimu wa kidato cha sita ambapo
walimtaka kuiweka ofisini kwake ili aendelee kuwakumbuka.
Picha Juu na Chini Mgeni rasmi
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi vyeti na zawadi kwa wahitimu wa
kidato cha sita wa St. Anthony katika sherehe za mahafali ya 20 shuleni
hapo.
Mstahi Meya Jerry Silaa akishow love na mmoja wa wanafunzi wanaohitimu aliyesoma kombi kama aliyosoma Mstahiki.
Mhitimu wa Kidato cha Sita Yvonne Laurent Mganga akipongezwa na familia yake baada ya kuhitimu kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya
Shule ya St. Anthony Bi. Fides Challe (wa tatu kushoto waliokaa), wageni
waalikwa pamoja na uongozi wa shule hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya burudani wa shuleni hapo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa na MC wa mahafali hayo ambaye ni Katibu wa wanafunzi Shuleni hapo Kennedy Mlawa.
Picha Juu na Chini wanafunzi wa St. Anthony ambao Mstahiki Meya Jerry Silaa ni Role Model wao wakionyesha upendo.
Bw. na Bibi Amos Bujiku na binti yao katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na Uongozi wa shule hiyo.
Ma soul was in that moment.....
ReplyDelete