Tuesday, February 26, 2013

   RONALDO AWAKALISHA BARCA:3-0
                     
kipaji maalumu toka Madeira,Christiano Ronaldo leo usiku aliendeleza balaa lake la kufumania nyavu ambapo aliwakalisha vijana wa Catalunya Barcelona ndani ya Camp Nou ambapo walikuwa wakigombania nafasi ya kucheza kombe la mfalme la HISPANIA yaani Copa Deley ambapo Barca hadi sasa wamekwishatolewa kufuatia uambatano wa magoli 4-2 baada ya gemu ya kwanza kutoka 1-1 Santiago Bernabeau jijini Madrid.
         Mapema Ronaldo aliipatia Madrid dakika ya 13 baada ya kukwatuliwa na Gerlad Pique bao ambalo lilidumu hadi dakika ya 57 ambapo aliongeza tena la pili kufuatia kazi nzuri aloifanya Angel Di Maria na baadaye kinda Rafael Varane alishindilia msumali wa tatu kufuatia mpira wa kona ulopigwa na Ozil dakika ya 67.
Baadaye Barca walipata bao la kufuatia machozi kupitia kwa beki wao Jordi Alba.
                  rafu iliyopelekea penati ya Ronaldo mapema dakika ya 13 ilozaa bao la kwanza baada ya Pique kumkwatua Ronaldo .   
                             Madrid wakishangilia bao la Rafael Varane.
Mpaka filimbi ya mwisho inalia Barcelona 1 Madrid 3.                                              
 
                        

No comments:

Post a Comment