Tuesday, February 26, 2013

VITUO VYA IMANI NA NEEMA FM VYAFUNGIWA KUTANGAZA HUKU CLOUDS FM IKITOZWA FAINI. 

                             mheshimiwa Walter Bgoya akiongea na waandishi  

                                               

Makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili ya utangazaji ndugu Walter Bgoya jana ameamuru vituo vya radio vya utangazaji vya TUMAINI na IMANI vifungiwe kufuatia ukiukwaji wa maadili ya utangazaji wa vyombo hivyo vya habari.vituo hivyo ambavyo vimefungwa  rasmi kutorusha matangazo yake kwa muda wa miezi sita mpaka itakapoisha.

          Akizungumza jijini Dar mheshimiwa BGOYA ameamuru pia Clouds Fm kufuata kipande cha Jicho la Ng"ombe kinachorushwa kupitia kipindi cha Power Breakfast chini ya Barbara Hassan na Paul James maarufu PJ kila siku asubuhi ambapo pia ameamuru watoe faini ya shilingi milioni tano taslimu ambapo hii inakuja baada ya kituo hicho kupewa lawama kuwa moja ya chanzo cha kwa nini wanafunzi wanapata matokeo mabaya hususani ya kidato cha nne.

Mwenyekiti Bgoya amefafanua zaidi kwamba vituo vya IMANI FM cha jijini Dar na NEEMA FM cha jijini mwanza kwa kosa la uchochezi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utangazaji nchini ambapo kituo cha Imani kinadaiwa kuchochea watu kutoshiriki katika sensa ya watu na makazi huku kile cha Neema kikidaiwa kuchochea mgogoro wa uchinjaji kati ya waislamu na wakristo mkoa wa Geita japo kamati hiyo ya maadili imeweka milango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa. 

                                            waandishi wa habari wakimsikiliza mheshimiwa huyo.
                         (picha kwa hisani ya www.thehabari.com)             

                                  

No comments:

Post a Comment