BENITEZ AITOSA CHELSEA
BENITEZ KUITOSA CHELSEA

Rafael Benitez,
amesema kuwa atakihama klabu ya Chelsea mwezi Mei mwaka huu na kutaja
uamuzi wa kuumpa wadhifa wa kaimu kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.
Akiongea
baada ya kuongoza Chelsea kushinda klabu ya Middlesbrough kwa magoli
mawili kwa bila katika mechi ya raundi ya tan ya kuwania kombe la FA,
kocha huyo kutoka Uhispania, vile vile aliwashutu mashabiki wa klabu
hiyo.
Katika mahojiano na BBC, Benitez amesema uamuzi wa Chelsea
wa kuumpa cheo cha kaimu kocha wa klabu hiyo ilikuwa kosa kwa sababu
yeye ndiye kocha mkuu kwa sasa.
Amesema mashabiki wao hawajawapa msaada wanaohitaji na hivyo ameamua kuondoka mwisho wa msimu huu.
'' Mashabiki sasa hawana sababu ya kunung'unika kunihusu'' Alisema kocha huyo.
Hatua
hiyo ya kocha huyo wa zamani wa Liverpool imekuja baada ya baadhi ya
mashabiki wa klabu huyo kumdhihaki baada ya mechi yao na Middlesborough.
Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 52, hajapata uungwaji mkono kutoka kwa
mashabiki wa klabu hiyo tangu alipoteuliwa kuchukua mahala pa Roberto Di
Matteo mwezi Novemba mwaka uliopita.
Na pia mwenendo mbovu wa Chelsea kwa sasa umewaletea mtazamo mbovu wa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake jijini London.
No comments:
Post a Comment