KIKWETE ATEMBELEA GHOROFA LILODONDOKA KARIAKOO
KIKWETE ALIPOTEMBELEA GHOROFA LA MAAFA.
Ni tukio la kuuzunisha na kusikitisha,Jengo la ghorofa 16 laporomoka katikati ya viunga vya Jiji la Dar
Rais Kiwete akiwa mitaa ya Hindira Ghandi jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es
salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe
jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo
hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa
kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi
zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo
lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia
Ithnaasheri
Mpaka sasa watu wawili inasemekana wamepoteza maisha na watu 17
wameokolewa ,zoezi la uokoaji waliofukiwa kwenye kifusi linaendelea kwa
juhudi, na uchunguzi wa nani anajenga na nani msimamizi
unaendelea
Rais
Jakaya Kikwete mchana huu ametembelea eneo lilipoanguka jengo la
ghorofa 16 katika makutano ya Barabara ya Zanaki na Indra Ghandi na
kuhimiza juhudi za uokoaji ziongozwe ili kuokoa maisha ya watu
wanasadikiwa kuwa wapata 60 waliofukikwa ndani ya Kifusi.Tayari askari
wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT) na lile la Wananchi(JWTZ) wapatao 500
wako eneo la tukio katika juhudi za uokoaji.
No comments:
Post a Comment