ROBIN VAN PERSIE KUSTAAFIA UNITED
Nyota mdachi anayekipiga United,Robin van Persie amesema anatarajia kumaliza soka lake katika klabu hiyo iliyoko jijini Manchester chini ya kocha Fergusson,straika huyo aliyesajiliwa mwaka jana kutoka kikosi cha washika bunduki wa London Arsenal the Gunners akimaliza msimu uliopita kama mfungaji bora.
Hali hii imekuja baada ya mdachi huyo kufunga bao mbili na kuiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Romania juzi na sasa kufikisha magoli 34 aliyoifungia timu yake ya taifa ndani ya michezo 74 huku akiwa ametupia mara 19 ndani ya ligi kuu ya Uingereza nyuma ya kinara wa ufungaji Luis Suarez akiwa na mabao 23.
Van Persie amedai hana mpango wa kuihama hiyo klabu hapo baadaye na kuahidi kwamba atastaafia hapo OLD TRAFORD pengine atakuwa akizifuata nyayo za mdachi mwenzio Edwin van der Sar aliyestaafia hapo klabuni mwak 2011.
No comments:
Post a Comment