MANDELA AZIDIWA NA KULAZWA TENA
MANDELA AZIDIWA TENA

Mandela alazwa tena hospitali!
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa hospitali
baada ya kupatwa tena na maambukizi katika mapafu yake. Hii ni mara ya
pili ndani ya mwezi huu kwa mwanaharakati huyo, shujaa wa kupinga
ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, kulazwa hospitalini.
Hapo Mwezi Disemba, Mandela alilazwa kwa wiki tatu hospitalini kwa
maambukizi kama hayo na upasuaji wa kuondoka uvimbe tumboni. Mapema
mwezi huu, Mandela alikaa hospitalini kwa usiku mmoja kwa ajili ya
uchunguzi wa afya yake.
Ofisi
ya Rais Jacob Zuma imesema madaktari wanaendelea kumhudumia, kuhakikisha
kuwa anapata matibabu bora zaidi ya kitaalamu na faraja. Mandela
amekumbwa na maradhi kadhaa yanayotishia afya yake katika miaka ya hivi
karibuni.
Mapema mwaka 2012 alilazwa kwa ajili ya uchunguzi
mdogo wa maumivu ya tumbo, na mwaka 2011 alilazwa kwa siku mbili
kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.
Blogu yetu inaungana na wasauzi wote katika kipindi hiki kigumu cha kumuuguza baba wa bara hili MADIBA OF THE PEOPLE,
Source: DW (Swahili)
No comments:
Post a Comment