Thursday, April 11, 2013

AZAM YAMKALISHA AFRICAN LYON

 AZAM WAZIDI KUMKIMBIZA YANGA KILELENI
            Timu ya soka ya Azam FC ya jijini Dar es salaam leo imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifumua timu ya African Lyon bao 3 bila katika mechi ilopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Azam Complex.
Alikuwa ni Khamis Ncha Vialli aliyeipatia Azam bao la kuongoza baada ya dakika kumi na nne za mchezo kuanza na baadaye alikuwa ni Kipre Tchetche aliyezamia msumali wa pili mnamo dakika ya 28 na hadi mapumziko Azam walikuwa mbele kwa bao mbili bila ambapo dakika 45 zote Azam walionyesha kuutawala mchezo huo.
         Kuunyesha walikuwa na njaa ya magoli mfungaji bora wa ligi kuu hadi sasa Kipre tchetche alizisalimia nyavu tena dakika ya 61 na hivyo kudhihirisha huenda akawa mfungaji bora wa msimu huu na mpaka filimbi ya mwisho Azam 3 African Lyon ya Zamunda 0                   

No comments:

Post a Comment