YANGA UTAIPENDA TU, YAICHAPA OLJORO 3-0

Young Africans imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri
ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom baada kufikisha point 52 bao 40
ya kufunga, pointi 6 mbele ya timu inayoshika nafasi ya pili Azam Fc
yenye pointi 46 huku timu zote zikiwa na michezo sawa 22.
Kikosi
cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika
ya 5 ya mchzo kupitia kwa mlinzi wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro'
aliipatia bao la kwanza kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona
iliyokuw aimepigwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Watoto
wa jangwani walionyesha kuwa wamedhamiria kupata ushindi mnono leo
kwani waliweza kucheza soka safi na la kuvutia huku Hamis Kiiza na
Didier Kavumbagu wakikosa mabao ya wazi ndani ya dakika 15 za kwanza.
Kiungo
chipukizi mwenye kasi Saimon Msuva aliipatia Young Africans bao pili
dakika ya 19 ya mchezo kufuatia kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya JKT
Olljoro na Msuva kumchambua kwa umaridadi mlinda mlango wa JKT Oljoro na
kuhesabu bao la pili kwa timu ya Yanga.
Yanga
iliendelea kulishambulia lango la JKT Oljoro muda wote wa mchezo na
mashuti ya washambuliaji wa Yanga yalimfanya mlinda mlnago huyo kutibiwa
mara kwa mara kwa kukoa michomo ya washambuliaji wa Yanga.
Dakka
ya 43, mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis Kiiza
aliipatia Yanga bao la tatu kufuatia mpira aliopenyezewa na kiungo Frank
Domayo na Kiiza kuwatoka walinzi wa JKT Oljoro na kuiandikia Yanga bao
la tatu.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ambapo waliingia Nizar
Khalfani na Said Bahanuzi kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu aliyeumia
na Simon Msuva mabadiliko yaliongeza ufundi zaidi na kuutalawa mchezo
kwa kipidndi chote.
Said Bahanuzi alifanyiwa
madhambi wakati akiwa ndani ya eneo la hatari akijandaa kumchambua
mlinda mlango wa JKT Oljoro lakini mwamuzi wa mchezo na mwamuzi wa
pembeni wake hawakujali na kuendelea na mchezo.
Zikiwa
zimebakia dakika tano kabla yakumalizika kwa mchezo, kiungo
mshambuliaji Nizar Khalfani alikosa bao la wazi kufuatia shuti lake
kuokolewa na mlinda mlango wake ambapo mpira huo ulipigwa kona ambayo
haikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro.

Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema anashukuru timu yake kupata kwa
ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza timu yangu ilicheza kwa
nguvu na kupata mabao ya mapema hali iliyoplekea kipindi cha pili
kucheza soka la burudani.
Timu imekua na
mabadiliko makubwa sana kiuchezaji na leo timu imecheza soka safi la
burudani lililoambatana na ushindi, hii ni zawadi kwa washabiki, wapenzi
wa soka na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa njia ya kutwaa ubingwa kwa
sasa ni nyeupe.
Yanga inajiandaa na mchezo dhidi
ya timu ya Mgambo Shooting siku ya jumatano mjini Tanga ambapo timu
itasafiri siku ya jumatatu tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao ni
muhimu kwa Yanga ili kuendelea kujiweka vizuri katika nafasi ya kutwaa
Ubingwa kabla ya kumalizika kwa msimu.
Young Africans:
1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul/Shadrack Nsajigwa, 3.David
Luhende, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani , 6.Athuman Idd
'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Didier
Kavumbagu/Said Bahanuzi,10.Hamis Kiiza, 11.Haruna Niyonzima(SOURCE,YOUNGAFRICANS.CO.TZ)
No comments:
Post a Comment