MWANAMKE AL;IYEDAIWA KUFARIKI MIAKA MITANO ILOPITA AFUFUKA
MWANAMKE ALIYEDAIWA KUFARIKI MIAKA MITANO ILOPITA AFUFUKA

Mwanamke anayedaiwa kufariki miaka mitano iliyopita Afufuka
MJI wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina
yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano
iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa. Inadaiwa kwamba
Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya
Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya
Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada
yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.
Aliyekuwa wa
kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya
kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke
aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama
huyo na marehemu dada yake.
“Baada
ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada
(Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba
nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia
anafanana na marehemu dada yetu,” alisema Jubili na kuongeza kwamba
alipowaita wote walitoka nje.
Alisema mtoto wa Flora (marehemu
anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba walimchukua
tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali ya
Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.
Rebeka ambaye ni mtoto wa nne wa Flora alisema: “Mama mdogo alituita
sisi tulikuwa tumelala akasema kwamba nje kuna mwanamke ambaye anafanana
na marehemu mama yetu, ndipo na sisi tukatoka na kweli kumwangalia
alikuwa ni yeye kabisa.”
Alisema walipomuhoji mama yake huyo
kwamba ametokea wapi, aliwaeleza kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga
na aliletwa na watu ambao hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya
gari na watu hao walimshusha kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni
jirani na dada zake hao.
Kauli ya Flora
Akizungumza na
waandishi wa habari, Flora alisema yeye ni mkazi wa Katoro na kwamba
alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi ambaye hata hivyo hakumtaja
kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini) wamemkataza.
“Nilikuwa
naishi kwa mganga wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati nikiwa pale
akaninywesha dawa kisha tukapakizwa kwenye gari na watu wawili ambao
sikuwatambua, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume mpaka hapa Kasamwa
tukashushwa saa 1:00 jioni,”alisema Flora.
Alisema alipofika
Kasamwa alikwenda kunywa uji kwa mama mmoja ambaye pia hakumtaja na
kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine saa nne usiku,
lakini watu wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia: “Hapa si kwako
twende tukupeleke kwa ndugu yako” na ndipo wakampeleka kwa dada yake
ambako aliketi nje hadi alfajiri.
Flora alisema kabla ya kuishi kwa
mganga alikuwa akiishi porini ambako alitupwa na watu asiowafahamu na
baadaye aliokotwa na wasamaria wema ambao ndiyo walimpeleka kwa mganga
ambako alikuwa akiishi muda wote(SOUCE;MWANZA CELEBRITY PAGE)
No comments:
Post a Comment