Wednesday, December 19, 2012

CHEKA KUKIPIGA ETHIOPIA

             CHEKA ULINGONI TENA
Bondia mtanzania toka Morogoro,Francis Cheka anatarajiwa kushuka ulingoni na bondia toka Malawi Chiotra Chimwemwe jijini Addis Ababa nchini Ethiopia hapo baadaye mwakani tarehe 26 Januari katika siku ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nchi za Afrika(AU SUMMIT).

                                 
Awali ya yote ikumbukwe kwamba Cheka na Chimwemwe watakutana Desemba 26 siku ya Boxing day katika kutafuta bingwa wa uzito wa SUPER MIDDLE WEIGHT katika bara la Afrika mashariki na kati na ghuba ya Uajemi(IBF AMEPG)katika pambano la raundi kumi na mbili(12),pambano hilo lililoandaliwa na Screen Hills(T)Investment ya jijini Dar es Salaam chini ya promota Andrew George a.k.a Chagga boy.Pambano hili limeshinikizwa makusudi kwa ajili ya kuchangia watu wenye njaa barani Africa.
Habari za kuaminika blogi yetu imezinasa toka kwa kamishna wa ngumi wa za kulipwa nchini HASHIM USTADH aliyeliidhinsha pambano hilo na hivyo wadau kukaa mkao wa kula kusubili pambano hilo hasa kwa wakazi wa Arusha kwani litafanyika huko Desemba 26 jijini hapo 





            

No comments:

Post a Comment