Wednesday, December 19, 2012

LULU ABADILISHIWA MASHITAKA

    KESI YA LULU YABADILISHIWA MASHTAKA

 
                 
Baada ya kuendelea kusota rumande kwa muda sasa msanii wa maigizo anayekabiliwa na kesi ya mauaji juu ya kifo cha msanii mwenzake marehemu Stephen Kanumba kilichotokea Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake Sinza Dar es salaam,Elizabeth Michael LULU amebadilishiwa mashtaka hivyo kuepuka adhabu ya kesi ya mauaji kama vile kunyongwa hadi kufa iwapo atakutwa na hatia.Hatua hii imekuja baada ya mkurugenzi wa mashtaka(DPP)kubadilisha mashtaka ya LULU hivyo kuwa KUUA BILA KUKUSUDIA kiasi cha lulu kuepuka adhabu kali ya mauaji hata kama akikutwa na hatia ambapo sasa lulu na kifungo cha maisha au kuachiwa huru kabisa.
Hali hii inambeba Lulu kutokana na kifungu cha 196 na kanuni za adhabu ya kosa la kuua bila kukusudia,ambapo anayepatikana na kosa la kuua bila kukusudia anaweza akakabiliwa na adhabu ya kufungwa miaka kadhaa,kifungo maisha au kuachiwa huru japo habari kutoka kwa wanasheria  wamedai kwa uzoefu wao adhabu nyingi za kuua pasipo kukusudia zilizowahi kutolewa nchini ukabiliwa na kifungo cha  miaka 15 na wengine huachiwa huru kabisa.
Lulu aliyefikishwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu tarehe 17/12/2012 jumatatu kufuatiwa awali alipofikishwa mahakamani Aprili 11 mwaka huu  na upande wa mashtaka kumweleza hakimu kuwa umeazimia na umembadilishia Lulu dhana ya mashitaka yake na kuwa kuua bila kukusudia kinyume na kifungu cha ICP namba 195.
Ilikuwa Lulu asomewe mashtaka yake siku hiyo mahakamani lakini hatua hiyo ilikwama kutokana na wakili mwandamizi wa serikali,TUMAINI KWEKA anayeendesha kesi hiyo kutokuwepo mahakamani na  badala yake kuwakilishwa na Wakili wa serikali Ofmedy Mtenga.
Ndipo wakili wake Lulu,Peter Kibatala alipoiomba mahakama itoe ahirisho fupi hadi Ijumaa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka haya mapya na hakimu Mbando alikubaliana na hili.  SOURCE;MWANANCHI

No comments:

Post a Comment