Christopher Katongo,captain wa timu ya taifa ya ZAMBIA maarufu kama CHIPOLOPOLO mabingwa watetezi wa Africa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji bora wa Africa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati baada ya kuwamwaga vinara wanaokiputa ulaya;Youness Belhanda wa Montpellier,Demba BA wa Newscastle,Didier Drogba wa Shanghai Shenhua na Yaya Toure wa Man City tuzo za hisani ya BBC ambazo hugaiwa kila mwaka.
katongo ambaye alifanya vyema na kuiongoza timu yake ya CHIPOLOPOLO kuibuka mabingwa wa AFCON kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira Africa wakiwaondoa Ivory Coast kwa penati alitangazwa majuzi kupitia BBC WORLD SPORTS SERVICE PROGRAMME kuwa ndiye aliyeibuka kidedea na tuzo yake iliwasilishwa kwa niaba ya BBC na mwakilishi wake bwana FANYI MUGANZI ambaye aliipeleka mikononi mwa mwenyekiti wa ZFA(Zambia Football Association) ndugu Kalusha Bwalya na ndiye aliyemkabidhi Katongo ambaye kwa sasa yuko kwenye kambi ya timu ya taifa akijiandaa na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya TANZANIA.
Katongo anayekipiga ligi kuu ya China Henan Constr japo awali aliwahi pita Butondo West Tigers,Kalulushi Modern Stars na Jomo Cosmos hakuwa mchoyo wa fadhila na alisema"NAWASHUKURU SANA WOTE MLIONIPIGIA KURA NA WADAU WOTE WA MPIRA KWA SAPOTI YENU PIA ALIISHUKURU TIMU ZIMA YA ZAMBIA PAMOJA NA Z.F.A PIA ALISISITIZA NI JUHUDI NDO ZILIZOMFIKISHA HAPO ALIPO HIVYO IWE CHANGAMOTO KWA WACHEZAJI CHIPUKIZI" .kingine tu ni kwamba katongo pia ni mwanajeshi na aliongezwa cheo baada tu kuisaidia Chipolopolo kuibuka na ubingwa ikiwa pia aliweka historia yeye na mdogo Felix Katongo kukipiga pamoja kwenye fainali za AFCON zilzofanyika Equitorial Guinea na Gabon.
No comments:
Post a Comment