Tuesday, December 18, 2012

WENGER AMLILIA STOPPILA SUNZU WA TP MAZEMBE

            STOPPILA ANAHITAJIKA ARSENAL
Beki  wa kati wa klabu ya Touit Pouissant Mazembe ya nchini Congo Stoppila Sunzu ambaye pia ni mdogo wa aliyekuwa mshambuliaji wa SIMBA ya Dar es Salaam Felix Sunzu,amekuwa lulu na kwa hali hiyo kuhitajika na klabu ya LONDON UINGEREZA Arsenal The Gunners inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo chini ya kocha mfaransa Arsen Wenger na Sunzu ndo tegemeo kuu la usajili wa Arsenal Wenger kipindi cha dirisha dogo kitakapofunguliwa yaani Januari mwakani. 
Stoppilla ambaye kwa sasa yupo kwenye kambi ya Chipolopolo akijiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Tanzania amesema"Ni kweli Arsenal kupitia kocha wake Wenger wameonyesha nia kumsajili na tayari kashaongea na mmiliki wa klabu yake ya sasa TP Mazembe Moisseau Katumbi juu ya hilo na keshamruhusu kuondoka hivyo anatarajia kwenda London kwa ajili ya mazungumzo ya uhamisho wake baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania tarehe 22/12/2012 itakayochezwa Dar es Salaam"Stoppila na Kalaba Reiford awali walitakiwa na timu moja ya Ubelgiji ila dili lao likafa baina ya kukosekana makubaliano kati Tp Mazembe na hiyo timu ya Ubelgiji.Jambo hili litakuwa bahati na chanzo cha kuendelea zaidi kwa soka la Zambia kwani ni matumaini Stoppila takuwa balozi mzuri na kuitangaza nchi yake kupitia soka la kimataifa na kama akifanikiwa kujiunga na Arsenal atakuwa mzambia wapili ndani ya EPL akijumuika na Emmanuel Mayuka wa Sunderland ambao wote ukijumuisha na wengine kama Katongo,Kalaba,golikipa wao Mwenne,Chisamba,Issack Chansa,Nkausu wametengeza majina na soko la vipaji vyao kutokana na soka la hali ya juu walolionyesha kipindi cha AFCON. 
Kila la kheri SUNZU.  
 

No comments:

Post a Comment