Watu 7 Wauawa Wakitoka Msikitini Kenya.
Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga
WATU saba wameuawa kwa kupigwa risasi katika
shambulizi karibu na msikiti Kaskazini Mashariki mwa Kenya, karibu na
mpaka na Somalia. Wanakijiji waliambia BBC kuwa watu kumi waliokuwa
wamejihami waliwashambulia kwa bunduki watu hao wakati walipokuwa
wanaondoka msikitini mapema asubuhi.
Taarifa zinazohusiana
Taarifa zinazohusiana
Mwanzo wanaume watano waliuawa na kisha wanawake wawili waliosikia
milio ya risasi walipofika kuchunguza, nao pia wakauawa. Shambulio
linafanyika chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika katika eneo
mojawapo ambapo usalama ni tatizo kubwa.
Wenyeji wa kijiji cha Malaley wanasema kuwa hakuna kilichoibiwa kwani
washambuliaji walitoroka punde baada ya shambulizi. Kijiji hicho kiko
umbali wa kilomita 45 kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo ni
makao kwa wakimbizi zaidi ya laki tano, waliotoroka vita nchini Somalia.
Katika mwaka mmoja uliopita, eneo hilo limekumbwa na mashambulizi
ambayo yamelaumiwa kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu Al Shabaab.
Al-Shabab iliahidi kulipiza kisasi wakati wanajeshi wa Kenya
walipokwenda Somalia kupambana nao, mwezi Oktoba mwaka 2011 kama juhudi
za kusaidia wanajeshi wa muungano wa Afrika.
-BBC
-BBC
No comments:
Post a Comment