Wednesday, April 17, 2013

Tz ya kijanja: MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-Mechi ya Lig...

Tz ya kijanja: MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-Mechi ya Lig...: MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/- Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uw...

BREAKING NEWZ;BI KIDUDE AFARIKI

    R.I.P BI FATUMA BINTI BARAKA
                       
BREAKING NEWS: R.I.P Bi.Kidude

Msanii nguli wa Muziki wa Taarab asili kutokea visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania, Fatuma binti Baraka maarufu kama Bi. Kidude amefariki dunia leo huko Zanzibar.

Monday, April 15, 2013

SIMBA,AZAM HAKUNA MBABE TAIFA

               SIMBA-2 AZAM-2
                                   


Ndoto ya Azam kuisogelea Yanga kileleni imeingia doa jana baada ya kulazimishwa sare 2-2 na Simba iliyoundwa na wachezaji chipukizi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi Simba walikuwa wa kwanza kupata mabao yao mawili kupitia mshambuliaji wao Ramadhani Singano kabla ya Azam kuamka na kusawazisha mabao kupitia penalti ya Kipre Tchetche na bao lililofungwa na Humpfrey Mieno.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi 47, wakati Yanga wakiwa kileleni na pointi 52, huku Simba wakibaki nafasi ya nne na pointi zao 36 na kupoteza matumaini ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa mwakani.
Katika mechi ya jana, Azam walianza mpira vizuri na kufanikiwa kufika langoni mwa Simba katika dakika ya kwanza baada ya shuti la John Bocco kutoka pembeni kidogo ya goli.
Simba walianza vizuri jibu mapigo baada ya mpira wa kona iliyopigwa na Mrisho Ngassa kutua kichwani mwa Shomari Kapombe, lakini kipa wa Azam, Mwadini Ally alikuwa makini kuokoa hatari hiyo.
Chipukizi Singano aliwainua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 11 akimalizia kazi nzuri ya Ngassa.
Wakati Azam wakiwa hawaamini kinachotokea Singano alifunga bao la pili katika dakika ya 18, baada ya Ngassa kumtoka beki wa Azam, David Mwantika na kupitisha pasi nzuri kwa chipukizi huyo.
Beki wa Azam, Mwantika alionekana mzito na kushindwa kwenda na kasi ya Ngassa na Singano waliomgeuza walivyotaka na kuipa Simba mabao mawili ya haraka.
Baada ya bao hilo kocha wa Azam, Stewart Hall alimtoa Luckson Kakolaki na kumwingiza Hamis Mcha katika dakika ya 20. Winga huyo alitumia dakika nane tu kabla ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki Miraj Mdigo na mwamuzi Oden Mbaga kutoa penalti iliyofungwa na Kipre Tchetche.
Kiungo wa kimataifa wa Kenya, Humpfrey Mieno aliisawazishia Azam bao katika dakika ya 71 akiunganisha vizuri mpira wa adhabu uliopigwa na Mcha baada ya Tchetche kufanyiwa madhambi na Said Nasoro Cholo.
Katika mechi hiyo, mwamuzi Mbaga alimtoa katika benchi, Kocha Hall na kumtaka aende kukaa jukwaani baada ya kumbwatukia akipinga uamuzi wake

MAN CITY YAFUZU FAINALI YA F.A CUP

      CHELSEA-1 MANCHESTER CITY-2
                                                
Samir Nasri mapema kipindi cha kwanza aliipatia Man City bao la kuongoza baada ya kutokea piga nikupige golini mwa Chelsea hali ilotokana na kazi nzuri ya kiungo wa City,Yaya Habib Toure kupandisha shambulizi nzuri hadi mapumziko City walikuwa mbele kwa goli moja.
 Aguero huyu akiwa na saikolojia nzuri baada ya kuwafunga goli zuri mahasimu wao Man utd wiki ilopita kwenye mechi ya ligi tena aliwapeleka kati Chelsea na kufanya matokeo kuwa mbili bila,baadaye mshambuliaji wa kimataifa wa Senegali Demba Ba aliwafungia Chelsea goli la kufutia machozi ambapo matokeo yalibaki vivyo hivyo hadi filimbi ya mwisho inalia.

MAN UTD AJIKITA ZAIDI KILELENI MWA LIGI KUU ENGLAND


 Mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa MAN UTD alikuwa mbele kwa bao mbili hali inayofanya timu hiyo yenye maskani katika jiji la Manchester kuzidi kuweka matumaini ya kuchukua ubingwa wa ishirini wa ligi kuu ya Uingereza chini ya kocha Sir Alex Fergusson,alikuwa ni Michael Carrick mapema katika kipindi cha kwanza na baadaye hakunaga Van magoli,mdachi Robin Van Persie aliyeshindilia msumali wa penati baada ya kukwatuliwa ndani ya eneo la hatari.
                                   


                                                

Pengine kilichovutia zaidi ndani ya mchezo ilikuwa baada ya dakika ya 76 Van persie kufunga bao la penati na hivyo kukata ukame wa mabao ulokuwa umemuandama karbia miezi miwili na kufikisha magoli ishirini nyuma ya kinara wa ufunga Luis Suares na kushangilia kwa nguvu kwa kumkumbatia kocha wake Alex Fergusson

                   

                                  

MWANAMKE AL;IYEDAIWA KUFARIKI MIAKA MITANO ILOPITA AFUFUKA

MWANAMKE ALIYEDAIWA KUFARIKI MIAKA MITANO ILOPITA AFUFUKA
                                                     
Mwanamke anayedaiwa kufariki miaka mitano iliyopita Afufuka

MJI wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa. Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.

Aliyekuwa wa kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada yake.
“Baada ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada (Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia anafanana na marehemu dada yetu,” alisema Jubili na kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka nje.

Alisema mtoto wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali ya Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.
Rebeka ambaye ni mtoto wa nne wa Flora alisema: “Mama mdogo alituita sisi tulikuwa tumelala akasema kwamba nje kuna mwanamke ambaye anafanana na marehemu mama yetu, ndipo na sisi tukatoka na kweli kumwangalia alikuwa ni yeye kabisa.”

Alisema walipomuhoji mama yake huyo kwamba ametokea wapi, aliwaeleza kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga na aliletwa na watu ambao hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya gari na watu hao walimshusha kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni jirani na dada zake hao.

Kauli ya Flora
Akizungumza na waandishi wa habari, Flora alisema yeye ni mkazi wa Katoro na kwamba alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi ambaye hata hivyo hakumtaja kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini) wamemkataza.
“Nilikuwa naishi kwa mganga wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati nikiwa pale akaninywesha dawa kisha tukapakizwa kwenye gari na watu wawili ambao sikuwatambua, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume mpaka hapa Kasamwa tukashushwa saa 1:00 jioni,”alisema Flora.

Alisema alipofika Kasamwa alikwenda kunywa uji kwa mama mmoja ambaye pia hakumtaja na kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine saa nne usiku, lakini watu wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia: “Hapa si kwako twende tukupeleke kwa ndugu yako” na ndipo wakampeleka kwa dada yake ambako aliketi nje hadi alfajiri.
Flora alisema kabla ya kuishi kwa mganga alikuwa akiishi porini ambako alitupwa na watu asiowafahamu na baadaye aliokotwa na wasamaria wema ambao ndiyo walimpeleka kwa mganga ambako alikuwa akiishi muda wote(SOUCE;MWANZA CELEBRITY PAGE)

Saturday, April 13, 2013

YANGA YAZIDI KUTETEA UBINGWA,YAIPIGA OLJORO

YANGA UTAIPENDA TU, YAICHAPA OLJORO 3-0





                               



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Young Africans imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom baada kufikisha point 52 bao 40 ya kufunga, pointi 6 mbele ya timu inayoshika nafasi ya pili Azam Fc yenye pointi 46 huku timu zote zikiwa na michezo sawa 22.

Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 5 ya mchzo kupitia kwa mlinzi wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' aliipatia bao la kwanza kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona iliyokuw aimepigwa na kiungo Haruna Niyonzima.
 
Watoto wa jangwani walionyesha kuwa wamedhamiria kupata ushindi mnono leo kwani waliweza kucheza soka safi na la kuvutia huku Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wakikosa mabao ya wazi ndani ya dakika 15 za kwanza.
 
Kiungo chipukizi mwenye kasi Saimon Msuva aliipatia Young Africans bao pili dakika ya 19 ya mchezo kufuatia kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya JKT Olljoro na Msuva kumchambua kwa umaridadi mlinda mlango wa JKT Oljoro na kuhesabu bao la pili kwa timu ya Yanga.
 
Yanga iliendelea kulishambulia lango la JKT Oljoro muda wote wa mchezo na mashuti ya washambuliaji wa Yanga yalimfanya mlinda mlnago huyo kutibiwa mara kwa mara kwa kukoa michomo ya washambuliaji wa Yanga.
 
Dakka ya 43, mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao la tatu kufuatia mpira aliopenyezewa na kiungo Frank Domayo na Kiiza kuwatoka walinzi wa JKT Oljoro na kuiandikia Yanga bao la tatu.
 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ambapo waliingia Nizar Khalfani na Said Bahanuzi kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu aliyeumia na Simon Msuva mabadiliko yaliongeza ufundi zaidi na kuutalawa mchezo kwa kipidndi chote.
 
Said Bahanuzi alifanyiwa madhambi wakati akiwa ndani ya eneo la hatari akijandaa kumchambua mlinda mlango wa JKT Oljoro lakini mwamuzi wa mchezo na mwamuzi wa pembeni wake hawakujali na kuendelea na mchezo.
 
Zikiwa zimebakia dakika tano kabla yakumalizika kwa mchezo, kiungo mshambuliaji Nizar Khalfani alikosa bao la wazi kufuatia shuti lake kuokolewa na mlinda mlango wake ambapo mpira huo ulipigwa kona ambayo haikuzaa matunda.
 
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro.

Wachezaji wa Young Africans wakimpongeza Saimon Msuva mara baada ya kufunga bal kwanza
Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema anashukuru timu yake  kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza timu yangu ilicheza kwa nguvu na kupata mabao ya mapema hali iliyoplekea kipindi cha pili kucheza soka la burudani.
 
Timu imekua na mabadiliko makubwa sana kiuchezaji na leo timu imecheza soka safi la burudani lililoambatana na ushindi, hii ni zawadi kwa washabiki, wapenzi wa soka na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa njia ya kutwaa ubingwa kwa sasa ni nyeupe.
 
Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Mgambo Shooting siku ya jumatano mjini Tanga ambapo timu itasafiri siku ya jumatatu tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ili kuendelea kujiweka vizuri katika nafasi ya kutwaa Ubingwa kabla ya kumalizika kwa msimu. 

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul/Shadrack Nsajigwa, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani , 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Didier Kavumbagu/Said Bahanuzi,10.Hamis Kiiza, 11.Haruna Niyonzima(SOURCE,YOUNGAFRICANS.CO.TZ)