Tuesday, February 26, 2013

         MAHAFALI YANGU YA KIDATO CHA SITA2013
Namshukuru sana Mwenyezimungu mpaka hapa nilipo na kwa hatua hii kubwa niliyofikia japo ni mwanzo wa safari lakini nashukuru sana na daima namuomba Jalali aninyooshee njia ili niweze kukamilisha ndoto ambazo nimekuwa nikiziota tangu awali na kitambo,EWE JALALI NAOMBA UNISAIDIE.
                                              Pia Shukrani zangu kwa Familia yangu,Mzee BITEGEKO,mama angu kipenzi ASHA ALLEY Bila kuwasahau ndugu zangu(MWAJUA,JAY 4,AHMED DEDY,YUSUPH,ABDULRAZAC NA ASHA BITEGEKO)  wote mmekuwa mstari wa mbele kuninyooshea mkono wa kheri na kuniombea angalau nifike hapa  najivunia nyie na Mungu awabariki sana.
                    Uongozi mzima wa ROCKEN HILL ACADEMY fika na Mkurugenzi wake Mr.A.KAZIMIL kwa sapoti kubwa tangu nkiwa mdogo mpaka leo jibaba nasema Ahsante sana palipo na walimu wangu walonifundisha advance level pale Anderlek,Mr.Adam,Japhary,Matiko,Nzumbi,rafiki yangu Mr.Dotto na  kaka angu RICHARD PAUL ambao wote wameniongoza kwa niaba ya walimu wote wa Anderlek hadi nahitimu sina cha kuwapa ila Mwenyezimungu ndo mpaji.
    Nikipokea cheti changu toka kwa mgeni rasmi wa mahafali yale ndugu SASA NELIGWA meneja wa benki ya AZANIA tawi la Kahama pembeni ya mama mkurugenzi mama angu mama ANATOLIA ALEXANDER na baba angu sir.ALEXANDER KAZIMIL.
                                     
                            PAMOJA NA MZEE BITEGEKO KUONYESHA NI JINSI ANAJALI KUHUSU ELIMU YANGU,BABA NASHUKURU.
C.E.O wa DAR CLASSIC WEAR kaka AHMED BITEGEKO hakuwa nyuma kuhakikisha mi na my twin bro ALLAN  V. FUNGO tunaifanisi siku kwelikweli tunashukuru sana kaka.
                                      Ahmed Bitegeko,Bitte Jr. na mwalimu wangu wa sayansi darasa la 5 Mr.Paul.
                   
                    Mzee Bitegeko,Uncle Edwin pamoja na Bitte Jr.Nashukuru sana wazee wangu.
            ALIPO SIDE NDO YUPO DULLAH..LOVE VERY MUCH BRO
                   Utajiri wa kwanza ni kuwa na marafiki,support kubwa ya maisha yangu elder homeboy Denis a.k.a Bosh,there Side a.k.a Cassanova,JJ a.k.a Chuma and lastly Bitte the poor billionaire.

   RONALDO AWAKALISHA BARCA:3-0
                     
kipaji maalumu toka Madeira,Christiano Ronaldo leo usiku aliendeleza balaa lake la kufumania nyavu ambapo aliwakalisha vijana wa Catalunya Barcelona ndani ya Camp Nou ambapo walikuwa wakigombania nafasi ya kucheza kombe la mfalme la HISPANIA yaani Copa Deley ambapo Barca hadi sasa wamekwishatolewa kufuatia uambatano wa magoli 4-2 baada ya gemu ya kwanza kutoka 1-1 Santiago Bernabeau jijini Madrid.
         Mapema Ronaldo aliipatia Madrid dakika ya 13 baada ya kukwatuliwa na Gerlad Pique bao ambalo lilidumu hadi dakika ya 57 ambapo aliongeza tena la pili kufuatia kazi nzuri aloifanya Angel Di Maria na baadaye kinda Rafael Varane alishindilia msumali wa tatu kufuatia mpira wa kona ulopigwa na Ozil dakika ya 67.
Baadaye Barca walipata bao la kufuatia machozi kupitia kwa beki wao Jordi Alba.
                  rafu iliyopelekea penati ya Ronaldo mapema dakika ya 13 ilozaa bao la kwanza baada ya Pique kumkwatua Ronaldo .   
                             Madrid wakishangilia bao la Rafael Varane.
Mpaka filimbi ya mwisho inalia Barcelona 1 Madrid 3.                                              
 
                WAZIRI PINDA ASHANGAA WANAOBEZA TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewaponda watu wanaoipinga tume aliyoiunda kuchunguza sababu za idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne kuvurunda katika mtihani huo akieleza kuwa huenda watu hao hawaelewi ukubwa wa tatizo na jinsi linavyotakiwa lishughulikiwe. Katika matokeo hayo ambayo yanatajwa kuwa mabovu kuliko yoyote yaliyowahi kutokea katika historia ya Tanzania, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo walipata sifuri.

Pinda alisema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa siku moja kuhusu mafanikio ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Alisema ni lazima waelewe kuwa mambo yatakayoangaliwa ndani ya uchunguzi huo ni mengi na si kama wanavyofikiri baadhi ya wanaopinga hivyo ni muhimu wakatulia na kusubiri matokeo.

“Wengine wanasema tume zipo nyingi, si kweli kwamba zipo nyingi na hazifanyi kazi, kila mtu ana mawazo yake, jambo hili ni kubwa na lazima lishughulikiwe kwa ukubwa wake,”alisema Pinda.

Pinda alisema hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kukamilisha tume hiyo na itaanza kazi kati ya leo au kesho.

“Tuko katika hatua za mwisho kwa kuwa tulihitaji kuhusisha wadau wote ikiwa ni pamoja na Zanzibar, dini mbalimbali, sekta binafsi pamoja na wabunge kadhaa ili tuunganishe nguvu na leo au kesho itaanza kazi rasmi,”alisema Pinda.

Wiki iliyopita Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo alisema kuwa tume hiyo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki hii, ambapo itajumuisha Chama cha Wamiliki wa Shule ya Sekondari na Vyuo Binafsi.

Lyimo aliwataja wadau wengine watakaohusika katika uchunguzi huo kuwa ni kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa)

“Tume hiyo itahusisha asasi zisizo za kiserikali (NGOs), zinazojishughulisha na masuala ya elimu. Wazazi, walezi na wananchi wote kwa jumla watoe ushirikiano kwa tume, ili ifanye kazi kwa ufanisi,” alisema Lyimo.
 
TFF Kujadili Kauli ya Serikali Kufuta Katiba Yake, Kocha wa Azam Afungiwa

Rais wa TFF, Leodger Tenga
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.
Baada ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu), Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo. Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
KOCHA Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.
Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.
Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
                                           
Watu 7 Wauawa Wakitoka Msikitini Kenya.

Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga
WATU saba wameuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi karibu na msikiti Kaskazini Mashariki mwa Kenya, karibu na mpaka na Somalia. Wanakijiji waliambia BBC kuwa watu kumi waliokuwa wamejihami waliwashambulia kwa bunduki watu hao wakati walipokuwa wanaondoka msikitini mapema asubuhi.
Taarifa zinazohusiana
Mwanzo wanaume watano waliuawa na kisha wanawake wawili waliosikia milio ya risasi walipofika kuchunguza, nao pia wakauawa. Shambulio linafanyika chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika katika eneo mojawapo ambapo usalama ni tatizo kubwa.
Wenyeji wa kijiji cha Malaley wanasema kuwa hakuna kilichoibiwa kwani washambuliaji walitoroka punde baada ya shambulizi. Kijiji hicho kiko umbali wa kilomita 45 kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo ni makao kwa wakimbizi zaidi ya laki tano, waliotoroka vita nchini Somalia.
Katika mwaka mmoja uliopita, eneo hilo limekumbwa na mashambulizi ambayo yamelaumiwa kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu Al Shabaab. Al-Shabab iliahidi kulipiza kisasi wakati wanajeshi wa Kenya walipokwenda Somalia kupambana nao, mwezi Oktoba mwaka 2011 kama juhudi za kusaidia wanajeshi wa muungano wa Afrika.
-BBC

  MKATABA WA AMANI CONGO WASAINIWA.

MKATABA wa kumaliza vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo leo umetiwa saini mjini Addis Ababa-Ethiopia na viongozi wa nchi za Maziwa Makuu. Viongozi wa nchi za maziwa makuu leo mjini Addis Ababa wameutia saini mkataba wa kumaliza vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo uliofikiwa kwa upatanishi wa Umoja wa Mataifa.
Viongozi hao walishindwa kuutia saini mkataba huo mwezi uliopita kutokana na mzozo juu ya nani anapaswa kukiongoza kikosi cha kulinda amani kitakachowekwa mashariki mwa Jamhuri ya Kongo.
Kutiwa saini kwa mkataba huo kutawezesha kuundwa kwa kikosi maalum cha jeshi la Umoja wa Mataifa kitakachoweza kuingilia kati katika eneo hilo la mashariki mwa Kongo na kupambana na waasi pamoja na kuanzisha juhudi mpya za kisiasa. Viongozi walioutia saini mkataba huo mjini Addis Ababa ni wa Msumbiji, Rwanda, Tanzania, Afrika Kusini, Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Sudan ya Kusini.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Nesirky ameeleza kuwa Umoja wa Afrika, mataifa 11 ya eneo la maziwa makuu, (ICGLR)pamoja na jumuiya ya wanachama 14 ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC,watakuwa “wadhamini wenza”.
Umoja wa Mataifa unatarajiwa kumteua mjumbe maalum atakaefuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo. Maofisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa hali ya kutokubaliana mwezi Januari ilitokana na wasi wasi juu ya taratibu, lakini sio kutokana na maudhui ya mkataba. Jason Stearns, mchambuzi anaefuatilia masualaya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, mapema mwezi huu aliyaita makubaliano hayo kuwa ni “hati isioeleweka kabisa.”
Amesema makubaliano hayo, yanalenga katika vipengere vitatu:”kuyazuwia mataifa ya eneo husika kujiingiza katika masuala ya ndani ya nchi nyingine, kuhimiza kufanyiwa mageuzi kwa taasisi dhaifu nchini Kongo na kuvutia uratibu bora zaidi wa wafadhili na ushiriki wao.
Eneo la mashariki mwa Kongo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini limevurugwa na makundi kadhaa yenye silaha katika muda wa miongo miwili iliyopita, huku makundi mapya ya waasi yakizuka kila mara, baadhi yao yakiungwa mkono na nchi jirani.
Ongezeko la hivi karibuni la machafuko lilitokea mwaka 2012 na kusababisha kuzuka kwa kundi la waasi la Machi 23, (M23) ambalo kwa muda liliuteka mji muhimu wa Goma Novemba mwaka jana. Kundi la M23 liliundwa na wapiganaji wa zamani wa kundi la waasi wa kabila la Watutsi ambao hapo awali waliingizwa katika jeshi rasmi la Serikali ya Congo kwa mujibu wa makubaliano ya amani, lakini wanadai kuwa masharti ya makubaliano hayo hayakutimizwa.
                               Mungu inua mkono wako na ulete amani huku.AMEN
 
VITUO VYA IMANI NA NEEMA FM VYAFUNGIWA KUTANGAZA HUKU CLOUDS FM IKITOZWA FAINI. 

                             mheshimiwa Walter Bgoya akiongea na waandishi  

Makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili ya utangazaji ndugu Walter Bgoya jana ameamuru vituo vya radio vya utangazaji vya TUMAINI na IMANI vifungiwe kufuatia ukiukwaji wa maadili ya utangazaji wa vyombo hivyo vya habari.vituo hivyo ambavyo vimefungwa  rasmi kutorusha matangazo yake kwa muda wa miezi sita mpaka itakapoisha.

          Akizungumza jijini Dar mheshimiwa BGOYA ameamuru pia Clouds Fm kufuata kipande cha Jicho la Ng"ombe kinachorushwa kupitia kipindi cha Power Breakfast chini ya Barbara Hassan na Paul James maarufu PJ kila siku asubuhi ambapo pia ameamuru watoe faini ya shilingi milioni tano taslimu ambapo hii inakuja baada ya kituo hicho kupewa lawama kuwa moja ya chanzo cha kwa nini wanafunzi wanapata matokeo mabaya hususani ya kidato cha nne.

Mwenyekiti Bgoya amefafanua zaidi kwamba vituo vya IMANI FM cha jijini Dar na NEEMA FM cha jijini mwanza kwa kosa la uchochezi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utangazaji nchini ambapo kituo cha Imani kinadaiwa kuchochea watu kutoshiriki katika sensa ya watu na makazi huku kile cha Neema kikidaiwa kuchochea mgogoro wa uchinjaji kati ya waislamu na wakristo mkoa wa Geita japo kamati hiyo ya maadili imeweka milango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa. 

                                            waandishi wa habari wakimsikiliza mheshimiwa huyo.
                         (picha kwa hisani ya www.thehabari.com)             

           MWAMUZI AONDOLEWA VPL

Mwamuzi Msaidizi wa FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya kupata alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au chini ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na FDL. 
Waamuzi wengine walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama (Yanga vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa Sugar).  
Walioondolewa kwa kupata alama za chini ni Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto Africans vs Coastal Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union), Idd Mikongoti (Toto Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs Mtibwa Sugar). 
Masoud Mkelemi aliyekuwa mwamuzi wa mezani katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad ameondolewa kwa kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na alichelewa kwa dakika tano kufika uwanjani.

               KOCHA WA AZAM AFUNGIWA.

Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.

Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.

Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers. 
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita. 
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. 
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana. 
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
 Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro. 
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea. 
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United. 
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki. 
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.

Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.

Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers. 
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita. 
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. 
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana. 
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
 Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro. 
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea. 
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United. 
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki. 
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

    TUKIO RASMI LA MSIBA WA GOLDIE.

Hatimaye msanii wa muziki na mshiriki wa BIG BROTHER AFRICA mwaka jana 2012 toka Nigeria OLUWABIMPE SUSAN GOLDIE HARVEY maarufu kama Goldie amezikwa leo kwenye makaburi ya vaults and Gardens Cemetery Ikoyi Lagos nchini Nigeria.Goldie ambaye alifariki mwezi uliopita tarehe 14 kufuatia shinikizo la damu kwenye ubongo aliletwa msibani hapo na gari aina ya Mercedez Benz R350 saa nne asubuhi. 
       Mazishi hayo ambayo yaliongozwa na aliyekuwa mme wa zamani wa Goldie Andrew Harvey yalifanyika jhuko Lagos na kuhudhuriwa na wageni waalikwa tu.
mwili wa marehemu saa chache kabla ya kuzikwa.
                                               Mme wa marehemu,Andrew Harvey akiwa katika mazishi ya mchumba na mke wake Goldie Harvey.

     mwili wa GOLDIE ukiwasili tayari kwa maziko.
                                                      
BLOGU INATOA POLE KWA WALE WOTE WALOGUSWA NA MSIBA HUU NA FAMILIA YA GOLDIE KWA UJUMLA,PUZIKA SALAMA
           REST IN PEACE GOLD HARVEY(1983-2013)
                                               
Sunday, February 24, 2013

MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA ST.ANTHONY 2012-2013

Mgeni rasmi katika mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa shule hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hizo.
Padri akiendesha ibada wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akifuatilia ibada hiyo kubariki mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John na Mkuu wa shule hiyo Bro. Ismail Edward ( wa pili kulia).
Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya St. Anthony wakisikiliza mahaburi wakati wa ibada hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kwenye sala maalum wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakisoma sala za mtu mmoja kuombea mambo tofauti ikiwemo Amani kwa Taifa.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari St. Anthony wakimwogoza mgeni rasmi kwa madoido ya aina yake wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya shule ya Sekondari St. Anthony akiwa ameambatana na viongozi wa shule hiyo tayari kuanza rasmi sherehe za mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakishiriki kuimba wimbo wa shule.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano wakiimba wimbo wa kuwaaga dada zao na kaka zao mbele ya mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari St. Anthony wakifanya igizo la Dr. Livingstone lililowavunja mbavu wazazi na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa hoi kwa kucheka kutokana na igizo la Dr. Livingstone. Kushoto ni Makamu Mkuu wa pili wa Shule hiyo Rempta Adams akifuatiwa na Mkuu wa Shule hiyo Bro. Ismail Edward.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo amezungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunza, mabadiliko ya mara kwa mara ya Mitaala na matamko juu ya Elimu, tabia ya wanafunzi kuiga tamaduni za Ughaibuni na Ukosefu/kukatika kwa nishati ya Umeme.
Sehemu ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akikabidhi taarifa ya shule yake kwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akisoma risala ya wanafunzi wa kidato cha sita mbele ya mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akimkabidhi mgeni rasmi risala hiyo.
Mwanfunzi Samwel Mwanzini akionyesha kipaji chake cha kuimba na kupiga kinanda ambapo alishangaza wengi kwa uwezo aliokuwa nao.
Mwanfunzi Tracy Raymond Ndanshau wa kidato cha tano PCM akiimba sambamba na Mwl. Nikiza Bwenge katika mahafali ya 20 ya kidato cha sita.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John (kulia) akisoma risala fupi ya kukabidhi wahitimu kidato cha sita 2013 kwa wazazi rasmi Bw. na Bibi Amos Bujiku wakati wa mahafali hayo.
Wazazi rasmi rasmi Bw. na Bibi Bujiku wakiwapokea rasmi wanafunzi Mary Bujiku na Edward Mugyabuso kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuwalea kiroho.
Mkuu wa Shule ya sekondari St. Anthony Bro. Ismail Edward akisoma risala kwenye mahafali ya 20 ya kidato cha sita ambapo amewasihi wanafunzi wanaohitimu waendelee kutunza kumbukumbu ya shule hiyo na kuwa mabalozi wazuri wa St. Anthony kwa kuwa wazalendo wa kweli waliotayari kulijenga na kulilinda taifa letu na kukabiliana na changamoto za dunia ya leo hususani gonjwa hatari la Ukimwi na matatizo mengine yanayoikumba Tanzania.
Meza kuu ipitia risala ya Mkuu wa shule hiyo.
Picha juu na chini Mgeni rasmi Mstahi Meya Jerry Silaa akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya St. Anthony ambapo ametoa pongezi kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo na kuongeza kuwa kwa sisi Watanzania Elimu ni nyenzo muhimu sana hasa katika mbio zetu za kupambana na maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini ambayo ni Silaha pekee ya kuwashinda maadui hao wote watatu.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Wahitimu wa kidato cha sita wakielekea kukabidhi zawadi kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea zawadi hiyo.
Mgeni rasmi akifingua zawadi hiyo mbele ya wahitimu hao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na wahitimu wa kidato cha sita ambapo walimtaka kuiweka ofisini kwake ili aendelee kuwakumbuka.
Picha Juu na Chini Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi vyeti na zawadi kwa wahitimu wa kidato cha sita wa St. Anthony katika sherehe za mahafali ya 20 shuleni hapo.
Mstahi Meya Jerry Silaa akishow love na mmoja wa wanafunzi wanaohitimu aliyesoma kombi kama aliyosoma Mstahiki.
Mhitimu wa Kidato cha Sita Yvonne Laurent Mganga akipongezwa na familia yake baada ya kuhitimu kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya St. Anthony Bi. Fides Challe (wa tatu kushoto waliokaa), wageni waalikwa pamoja na uongozi wa shule hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya burudani wa shuleni hapo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa na MC wa mahafali hayo ambaye ni Katibu wa wanafunzi Shuleni hapo Kennedy Mlawa.
Picha Juu na Chini wanafunzi wa St. Anthony ambao Mstahiki Meya Jerry Silaa ni Role Model wao wakionyesha upendo.
Bw. na Bibi Amos Bujiku na binti yao katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na Uongozi wa shule hiyo.